Ticker

6/recent/ticker-posts

Polisi aua wenzake, ajiua kwa risasi Kenya

MARSABIT-Afisa wa Jeshi la Polisi nchini Kenya leo Oktoba 23,2022 amejiua kwa risasi dakika chache baada ya kuwapiga risasi wenzake wawili katika Kituo cha Polisi cha Moyale, Kaunti ya Marsabit.

Maafisa kutoka DCI eneo husika.(Picha na Kenyans.co.ke).

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyoonwa na wavuti ya Kenyans imeeleza kuwa, afisa huyo aliiba bunduki hiyo kutoka kwa mwenzake kabla ya kuelekea kwenye hifadhi ya silaha ambapo aliwaua polisi wengine wawili.

"PC Lawrence alichukua jiwe kubwa na kumpiga PC Orero kwenye paji la uso akachukua bunduki yake kabla ya kukimbilia kwenye ghala la silaha ambapo maafisa wengine walikuwa wakichukua silaha kwa kazi ya siku hiyo.

"Alipiga risasi katika safu ya wasimamizi, na kumuua papo hapo na pia kumfyatulia risasi PC Matete,"imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Aidha, Afisa wa tatu alipata jeraha la risasi katika mkono wake wa kushoto. Kisha afisa huyo alirudi nyumbani kwake, ambako alijichomoa.

"PC Kumber kisha akarudi nyumbani kwake ambapo alifunga mlango kwa ndani na kujipiga risasi kidevuni," ilisomeka taarifa hiyo kulingana na kitabu cha matukio (OB Namba 09/23/10/2023).

Miili ya marehemu imesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Moyale. Huku, maafisa wawili waliojeruhiwa wakikimbizwa katika Hospitali ya Alhilal. Kulingana na polisi, askari aliyepigwa risasi mikononi mwake yuko katika hali mbaya.

Post a Comment

0 Comments