Ticker

6/recent/ticker-posts

DIARRA AIBEBA YANGA SC, IKIICHAPA KAGERA SUGAR 1-0


*****************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeendeleza ubabe kwenye ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar 1-0 kwenye mchezo ambao uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Yanga Sc imepata bao kupitia kwa nyota wao kinda kabisa Clement Mzize ambaye alipokea krosi nzuri kutoka kwa Feisal Salum katika kipindi cha kwanza cha mchezo na kuisadia timu yake kuibuka na ushindi huo muhimu.

Yanga Sc iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wao akiwemo Morrison, Bangala,Aucho na Moloko na kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao mara nyingi huwa hawachezi mara kwa mara..

Post a Comment

0 Comments