Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI KIGAMBONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia maji baada ya kuwasha mtambo (pampu) wa kutoa maji chini ya ardhi kwenye kisima kirefu (m 450) kwa ajili ya kuyapeleka kwenda kwenye tanki kubwa la maji katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuwasha mtambo (pampu) wa kusukuma maji kwenye tanki kubwa la maji kwa ajili ya usambazaji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusiana na mradi mkubwa wa maji ya visima 7 ambao unatoa maji zaidi ya lita milioni 70 kwa siku kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuzindua Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni tarehe 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi na ugawaji wa magari ya mitambo kwa ajili ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo, Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kuzindua na kugawa magari ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa lita milioni 70 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi pamoja na Wananchi baada ya kuzungumza nao kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa lita milioni 70 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam 11 Novemba, 2022.

Wananchi wa Kigamboni pamoja na maeneo jirani wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Post a Comment

0 Comments