Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA UWAJIBAKAJI UNAOZINGATIA SHERIA SEKTA YA ARDHI

Na Munir Shemweta, WANMM

Naibu waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema watumishi wa sekta ya ardhi nchini wanao wajibu katika utendaji kazi na dhana nzima ya kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia sheria.

"Tunahitaji nidhamu na miongozo mbalimbali ili kutoa hiduma stahiki kwa watanzania.

Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleio ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema hayo tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi.

Aidha, amesema mwajiri naye anao wajibu wa kuweka mazingira mazuri mahali pa kazi sambamba na kuwaheshimu watumishi na kuwaendeleza ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela, Naibu Waziri Pinda alisema mpango wa urasimishaji unafikia kikomo mwaka huu wa 2023 na makazi holela yanaendelea kushamiri huku miji ikikua kwa kasi.

Kwa mujibu wa Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, kazi ya Baraza la Wafanyakazi ni kutumia mkutano huo wa Baraza kuishauri serikali juu ya mkakati mpya wa kuondoa makazi holela.

Amelitaka Baraza la Wafanyakazi kujadili kwa kina makadirio ya mipango ya matumizi kwa mwaka 2023/2024 na kuweka mipango inayotekelezeka.

Pamoja na mambo mengine ametaka kuwekwa mikakati madhubuti kwenye masuala ya makusanyo ya kodi ya ardhi ambapo amesema wizara imekusanya bil 129 sawa asilimia 51.6 ya lengo jambo alilolieleza halikubalikia.

Ameelekeza kila mkoa kuongeza kasi ya makusanyo ili kutimiza lengo lililowekwa na kuchukua hatua kwa wadaiwa wote sugu kutokana na muda wa msamaha wa rais kupita.




Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa kikoa cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara yake tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma.

Post a Comment

0 Comments