Ticker

6/recent/ticker-posts

TPA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 10 HOSPITALI YA WILAYA KIGAMBONI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA imetoa msaada wa Shilingi Milioni 10 kusaidia ujenzi wa uzio katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 18 ya Mamlaka hiyo.
Akikabidhi Msaada huo ulioambatana na zoezi la Upandaji miche ya matunda zaidi ya 200 na kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo umekabidhiwa kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kigamboni na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mrisho S. Mrisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa

Mrisho amesema, TPA itaendelea kusaidia jamii inayozunguka kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii katika maeneo ya Elimu , Afya , Maendeleo ya Jamii na Majanga kulinga na Sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR )pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma kwa jamii.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu ameishukuru TPA kwa kuguswa na kutoa kwa jamii kwa lengo la kusaidia kuboresha huduma za kijamii hasa katika Afya na Elimu. Kadhalika ametumia fursa hiyo kuzirai Taasisi zingine kuiga mfano wa TPA kutoa sehemu ya faida ya Taasisi zao ili kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za Jamii.

Kiasi hiko cha milioni 10 kilichotolewa na TPA ni kwaajili ya kusaidia ujenzi wa uzio katika hospital hiyo Kwa lengo la kulinda usalama wa watendaji wa afya na wagonjwa.

Post a Comment

0 Comments