Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI AWESO AFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU WA MAJI WANAOTEKELEZA MIRADI KWENYE MIJI 28 TANZANIA

NEW DELHI, INDIA

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa nchini India kwenye ziara ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya Maji hususani viongozi wa makampuni ya wakandarasi wanaotekeleza Mradi mkubwa wa Maji nchini Tanzania wa MIJI 28 ukumbi mdogo wa ITC MAURYA Hotel.

Waziri Aweso aliembatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Jamal Katundu na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini India Bwana Deo Dotto sambamba na Mkurugenzi Msaidizi Wa Rasilimali za Maji Bwana Robert Sunday amesisitiza Mradi huu kukamilika kwa wakati kwani watanzania wana matumaini na matarajio makubwa ambao unatarajiwa kukamilika mwaka 2025.

Waziri Aweso akizungumza na Wakandarasi wote wa Mradi pamoja na Mkandarasi Mshauri na mwakilishi wa Benki ya Exim na Wizara ya Maji India ameeleza ni kwa namna gani Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyowezesha kukamilika kwa michakato ya Mradi huu kuanza baada ya kuchukua muda mrefu akiwahimiza kuifanya kazi hii vizuri kama kurejesha shukrani kwake na kutimiza ufanikishaji wa malengo yake ya ajenda ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.

Aidha Waziri Aweso amewaahidi ushirikiano katika hatua zote katika kipindi hiki ambacho utekelezaji wa Mradi unaendelea.

Katika hatua nyingine wadau wamemshukuru Waziri Aweso na Katibu Mkuu Prof.Katundu kwa kuridhia kukutana nao na kuwasikiliza changamoto zao na kutoa majibu pamoja na ushirikiano mzuri wanaopata wakati wote toka kwa Wizara ya Maji.

Mwisho Kwa pamoja wameahidi kuongeza kasi na kuifanya kazi hii ya Utekelezaji wa Mradi wa Maji 28 kwa ufanisi na ubora.


Post a Comment

0 Comments