Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZEE WA KIMILA, MACHIFU WAOMBWA KUSHIRIKI MAPAMBANO VITA DAWA ZA KULEVYA KUIKOA JAMIII

Na Mwandishi Wetu

KAIMU Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Kanda ya Kati Christian Mbwasi amewaomba wazee wa kimila na Machifu nchini, kwa nafasi zao kupinga matumizi ya dawa za kulevya, ili kuiokoa jamii.

Pia, amewataka kuukumbusha umma juu ya athari za kujihusisha na matumizi au kilimo cha bangi na mirungi hali inayohatarisha ustawi wa taifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi hao kutoka Kanda ya Kati Dodoma na Kanda ya Pwani kwa mkoa wa morogoro pamoja na Zanzibar, aliposhiriki sherehe za kimila zilizofanyika viwanja vya machifu eneo la Bwibwi - Jedengwa mkoani Dodoma alipokuwa akitoa salamu za DCEA.

Amesema, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, inaamini kupitia sauti za wazee wa kimila, kwa umoja wao wataweza kuiokoa jamii kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya.

"Nyinyi ni viongozi wa jamii, tunaamini kwa kupitia sauti zenu ujumbe wetu utafika kwa haraka kuhusiana na kuitaka jamii kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya...hivyo tunaomba ushirikiano wenu katika hili, ili jamii iondokane na matumizi na ununuzi wa dawa za kulevya",amesema Mbwasi.

Kwa upande wake, Ofisa Utamaduni Jiji la Dodoma, Dezdel Ruzenza, ameiomba Mamlaka kuendesha majukwaa ya kutoa elimu kuhusiana na dawa za kulevya kufanyika mara kwa mara.

Awali Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Pick Foundation Shiganga George amesema, taasisi hiyo inaunga mkono jitihada zinazoendelea kufanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, kupitia Kamishna Jenerali Aretas Lyimo, ambaye ameendelea kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na kuwachukulia hatua wale wote wanaobainika kutumia na kuuza dawa hizo.

Pia, ameipongeza Mamlaka hiyo, kutumia nafasi hiyo ya kukutana na wazee wa kimila, kuwataka kutumia nafasi zao katika jamii kukemea vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya ili kuokoa in matumizi ya dawa za kulevya, kwa umoja wao watatumia vikao vyao kuelimisha vijana kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya.






Post a Comment

0 Comments