Ticker

6/recent/ticker-posts

MHE. PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA WIZARA YA ARDHI URU-MOSHI

Na Munir Shemweta, MOSHI

Naibu Waziŕi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameshiriki katika mazishi ya mtumishi wa Wizara ya Ardhi Makao Makuu Joyce Shayo.

Mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera yamefanyika katika eneo la Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Desemba 2024.

Marehemu Joyce Shayo amefariki tarehe 30 Desemba 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam akisumbuliwa na Shinikizo la Damu.

Marehemu atakumbukwa zaidi kwa kuwa sehemu ya timu ya wataalamu waliokuwa wakifanya kazi ya Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975. Marehemu ameacha watoto watatu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi wakiwa na familia ya marehemu Joyce Shayo wakati wa mazishi yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Wizara ya Ardhi Joyce Shayo wakati wa mazishi yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda na Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera wakiwa na familia ya marehemu Joyce Shayo wakati wa mazishi yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda na Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera wakiweka shada la maua wakati wa mazishi ya marehemu Joyce Shayo yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi wakiweka shada la maua wakati wa mazishi ya marehemu Joyce Shayo yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024
Watoto wa Marehemu wakiweka shada la Maua wakati wa mazishi ya mama yao Joyce Shayo.
Wazazi wa Marehemu Joyce Shayo wakiweka shada la Maua.
Sehemu ya waombolezaji katika msiba wa Joyce Shayo (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Post a Comment

0 Comments