Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU GDSS WATOA SABABU ZA KUSHINDWA KWA WANAWAKE KUSHIRIKI KWENYE MCHAKATO WA UCHAGUZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANAHARAKATI wa jinsia na wadau wa semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) wameendelea kupaza sauti zao kuhusiana na sababu zinazochangia,kwa kiasi kikubwa Mwanamke kushindwa kushiriki katika Mchakato uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wahabari leo Januari 24,2024 katika makao makuu ya mtandao wa Jinsia nchini (TGNP),Mabibo- Jijini Dar es Salaam Mdau wa masuala ya kijinsia kutoka kata Mbulahati Bw.Alan Christopher amesema mkwamo ambao watu wametoa shuhuda ni pamoja na imani za kishirikina ambapo kumekuwepo na hali yakutokuwa na ukomo wa kuongoza.

"Changamoto kubwa ambayo imeonesha ni kujirudia kwa kiongozi mmoja ni jambo baya sana na linakwamisha masuala ya junsia hata watu wenye changamoto mbalimbali"Bw.Alan amesema.

Aidha Bw.Alan ameeleza kuwa mabadiriko ya Sheria za uchaguzi ndio suluhisho kubwa la kutatua changamoto ya kujirudia kwa mtu mmoja kuongoza kwa muda mrefu ambapo itachagiza maendeleo kwa kupata kiongozi mwenye maono mapya.

Kwa Upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia kutoka kata ya Mwabepande Bi.Catherine Massawe amesema kuwa moja ya changamoto ya ushiriki wa Wanawake katika Uongozi ni swala la fedha,rushwa ngono,Pamoja na nidhamu ya Uoga kutokana na Mila na desturi.

Amesema wanawake wanatakiwa kupewa elimu kuondoa hofu ya kuwa viongozi ili wapate ujasiri na kwa wanaume waweze kutambua mwanamke anaweza kuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa.

Naye Mdau wa semina za Jinsia Bi.Mpegwa Noah kutoka Kata Mianziani ameeleza kuwa amejifunza kuwa mwanamke anatakiwa kuwa imara na kuishi kwa upendo pamoja na kujiweka karibu na jamii ambapo itamsaidia katika kugombea Uongozi na kueleweka kwa watu.

Post a Comment

0 Comments