
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bi. Rose Joseph, akitoa Maelezo kuhusu ushiriki wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.
Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,ametembelea Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Nne (4) cha Serikali Mtandao eGA, kilichoanza leo mkoani Arusha.
Mhe. Simbachawene, amepongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikj, pamoja na ubunifu mzuri wa Wanafunzi kutoka Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Angavu(CIVE).
Chuo Kikuu cha Dodoma ni miongoni mwa wadhamini wa Mkutano wa Nne wa Serikali Mtandao, unaokutanisha Wakuu wa Taasisi, Maafisa TEHAMA, Wakurugenzi wa Mipango, Utawala, na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini. Kikao hicho kimeanza leo Jumanne tarehe 06 Februari na kinategemewa kumalizika Ijumaa tarehe 08 Gebruari 2024.




0 Comments