Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDUMBARO AFANYA ZIARA TaSUBa

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amefanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na kujionea maendeleo mbalimbali ikiwemo ukarabati wa miundombinu.

Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo leo Machi 26, 2024, Dkt. Ndumbaro amesema amefurahishwa na utoaji wa elimu ya sanaa katika taasisi hiyo ikiwemo kuvuka malengo ya kufanya udahili wa wanafunzi wapya katika vipindi vya hivi karibuni.

Aidha Dkt. Ndumbaro amesema kuwa serikali imetenga bajeti ya sh. Bilioni 1.5  kuhakikisha inaboresha zaidi tasnia ya sanaa ikiwemo taasisi ya TaSUBa.

Amesema Serikali inajipanga kuanzisha mashindano ya sanaa na burudani katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA ambapo washindi watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kufanya ziara TaSUBa na kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa sekta hiyo.

“Nimefurahishwa na utendaji wa kazi hapa TaSUBa ikiwemo uongozi kuvuka malengo kwa kufanya udahili wa wanafunzi wengi zaidi tofauti na ilivyotarajiwa.

“Serikali imetenga kiasi cha fedha cha sh. bilioni 1.5 katika sekta ya sanaa ikiwemo kusaidia kurekebisha miundombinu ya TaSUBa na kununua vifaa vipya vya kufundishia". Amesema 

Naye Mkuu wa Taasisi ya TaSUBA, Dkt. Herbert Makoye amesema wanaishukuru serikali kwa kuongeza bajeti katika mwaka ujao wa fedha, hivyo wanatarajia fedha zitakazotolewa zitasaidia kuendeleza miundombinu ikiwemo kukarabati majengo na kununua vifaa vya kufundishia.

 “Tunaishukuru serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutambua mchango wa sanaa nchini, tuna imani fedha zitakazotolewa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha, zitatumika kuboresha miundombinu na kununua vifaa vya kufundishia,” amesema Dkt. Makoye.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro akimsikiliza Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye  mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro akikagua studio za redio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro akijaribu kutumia kamera ya picha mjongeo inayotembea wakati alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro akimsikiliza Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye  mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye wakiongea na walimu wa Taasisi hiyo mara baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara TaSUBa leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro akikagua Camera ambayo ni moja ya vifaa ambavyo amekutana navyo katika studio za  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)  mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro akikagua studio za redio za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye wakiwa katika studio za Taasisi hiyo mara baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara  TaSUBa leo Machi 26, 2024.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro akiwa pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye wakishuhudia mazoezi ya uimbaji kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo mara baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara TaSUBa leo Machi 26, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments