Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE, WIZARA YAIPONGEZA ASAS UZALISHAJI WA MAZIWA BORA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, leo zimeipongeza kampuni ya Asas katika kuzalisha bidhaa bora za maziwa, hii ni mara baada ya kamati hiyo pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutembelea kiwanda Asas cha uzalishaji maziwa zikiwa na lengo la kujua mafanikio na changamoto za Uzalishaji bidhaa hizo za maziwa.

Akizungumza, leo Juni 14, 2024 Mkoani Iringa, Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika, amesema nia ya kamati ya Bunge ilikuwa ni kutembele na kuona mchakato mzima wa uzalishaji wa maziwa. Na kwenye hii ziara, kamati ya Bunge imejifunza mengi na kusikiliza mafanikio na changamoto za uzalishaji maziwa. Na kuelezea kuwa wao kama washauri na wasimamizi wa serikali hii itawapelekea kujua nini hasa wafanye kwenye Tasnia ya maziwa.

Aidha Mhe. Mwanyika aliendelea kusema kwenye maziwa angalau nchi sasa inazalisha. Na nia ya kamati ya Bunge ni kulinda viwanda vya uzalishaji maziwa kwa sababu tasnia ya maziwa ina matokeo kwenye maisha ya watu kiujumla. Na kama kamati wanaangalia bajeti isiwe kikwazo kwenye sekta hii ya maziwa na ndio mana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliweka sekta hii inayojitegemea peke yake, na wao kama kamati wamelipokea hili na watatafakari.

"Ni uwekezaji mkubwa, unaofaa na unaotoa ajira. Na inakidhi kwa kila nyanja na ni vyema kuisaidia hii tasnia ya maziwa kama ina changamoto. Na kwa hiyo tunawapongeza sana Asas kwa kuzalisha maziwa bora" Mhe. Mwa yika amesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amesema mifugo nchi Tanzania inachangia asilimia 7% ya pato la Taifa, na ndani ya 7%, asilimia 30% inatokana na maziwa.

Prof. Shemdoe aliendelea kusema kuwa tasnia ya maziwa ni tasnia kubwa sana ambayo lazima ipewe kipaumbele. Nchini kuna ng'ombe wa maziwa milioni moja na tatu ambao ng'ombe hawa wanatoa maziwa lita bilioni 3.9. Lakini katika maziwa hayo bilioni 3.9, kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wa Asas, ni asilimia 3% tu ambayo yanakwenda kwenye biashara za viwandani, ila asilimia 97% yanauzwa mtaani kwenye chupa za Maji.

"Haya maziwa lita bilioni 3.9 tukiweka katika mfumo wa hela inatupa thamani ya shilingi Trioni 7.8 kwa mwaka. Hii ionekane ni kwa namna gani Tasnia ya maziwa inavyochangia pato la Taifa kwa hali ya juu." Prof. Shemdoe alisema

Prof. Shemdoe aliendelea kusema Tanzania tuna viwanda jumla 152 ambavyo ni viwanda vidogo na viwanda vya kati na sita tu ndio vikubwa kimoja wapo cha Asas . Na katika hivyo viwanda 152, Asas ndio kiwanda pekee kilichoanza uzalishaji maziwa ya unga ingawa tunatumia kiasi cha Dola milioni 8.1 kuingiza maziwa ya unga kwa mwaka nchini. Japo soko tulilonalo la ndani kama tunaweza hakikisha tunazalisha maziwa ya unga kwa wingi.

"Hawa wenzetu wa Asas walivyoamua kulianza hili, sisi tuliona ni jambo jema na kubwa sana na ndio mana tunawaunga mkono" amesema Prof. Shemdoe

Akielezea mafanikio na changamoto katika uzalishaji wa maziwa katika kiwanda cha Asas, Mkurugenzi Mtendaji wa Asas, Bw.Fuad Asas, akianza na mafanikio amesema, mwaka 2000 Asas ilianza uzalishaji ikiwa na lita 1000 na wafugaji 50, lakini leo hii ipo katika uzalishaji wa lita 350,000 na wafugaji 9500 na ina wafanyakazi 400.

"Tunakusanya maziwa katika mikoa mitatu, Mbeya, Iringa na Njombe. Na tunajivunia kuwa kiwanda chenye bidhaa nyingi ambao ni mtindi, yogurt, cheese, pamoja na maziwa ya unga katika viwanda vyetu vyote viwili." amesema Bw. Asas

Aliendelea kusema Asas wameweza kusambaza madume bora Njombe na Makambako, na kutoa elimu ya ufugaji kibiashara kwa wafugaji pamoja na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya unga.

"Moja ya changamoto kubwa ni unywaji maziwa ni asilimia 28% tu, unywaji wa maziwa ni duni kwa sababu ya uelewa. Na hatuwezi peleka bidhaa nje ya nchi kwa sababu hakuna sera ya kuthibiti magonjwa." amesema Bw. Asas
Mwakilishi wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kulia), akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Mhe. Joachim Nyingo (wa tano kulia), baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika (kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, akisalimiana na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Mhe. Joachim Nyingo (katikati), baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika (wa tatu kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mfugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kulia), baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika (aliyesimama), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, akijitambulisha kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Mhe. Joachim Nyingo (aliyekaa) na kuelezea nia na dhumuni la ujio wa Kamati ya Bunge ya kudumu katika Mkoa wa Iringa, baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa ajili ya Utambulisho na kuelezea nia na dhumuni la ujio wao Iringa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakitembelea kiwanda cha uzalishaji maziwa cha Asas, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mkurugenzi Mtendaji wa Asas Dairies Ltd, Bw. Fuad J. Abri (Asas), akielezea mafanikio na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika uzalishaji wa zao la maziwa, wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo walipotembelea kiwanda cha hicho ili kujua changamoto na mafanikio katika uzalishaji wa zao la maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mwakilishi wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (aliyesimama), akielezea ukubwa wa Tasnia ya maziwa na faida yake, baada ya kuwasili katika kiwanda cha Asas kujionea shughuli za uzalishaji maziwa na mafanikio yake pamoja na changamoto za uzalishaji maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika (aliyesimama), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,  akielezea akielezea mchango wa Asas katika Tasnia ya Maziwa, mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha Asas kujionea shughuli za uzalishaji maziwa na mafanikio yake pamoja na changamoto za uzalishaji maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mkurugenzi Mtendaji wa Asas Dairies Ltd, Bw. Fuad J. Abri (wa pili kulia), akielezea Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo mchakato mzima wa uzalishaji wa maziwa ya unga katika kiwanda cha Asas, punde Kamati ya Bunge walipotembelea kiwanda hicho ili kujua changamoto na mafanikio katika uzalishaji wa zao la maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakitazama bidhaa za zao la maziwa zinazozalishwa na kiwanda cha Asas, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mkurugenzi Mtendaji wa Asas Dairies Ltd, Bw. Fuad J. Abri (kulia), akimkabidhi maboxi ya bidhaa mbalimbali za maziwa, Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika (kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, wakati Kamati ya Bunge walipotembelea kiwanda hicho ili kujua changamoto na mafanikio katika uzalishaji wa zao la maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Mbunge, Mhe. Salma Kikwete, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza ziara ya ujio wa Kamati ya Bunge katika kiwanda cha Asas kwa lengo la  kujionea shughuli za uzalishaji maziwa na mafanikio yake pamoja na changamoto za uzalishaji maziwa, leo Juni 14, 2024, Iringa
Picha ni sehemu ya watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakiwa kwenye picha ya pamoja walipotembelea kiwanda cha Asas kuangalia uzalishaji wa zao la maziwa ikiwa na kujua mafanikio na changamoto zake katika uzalishaji, leo Juni 14, 2024, Iringa
Picha ni sehemu ya aina ya ng'ombe wafugwao katika kiwanda cha maziwa cha Asas wakiwa katika zizi Juni 14, 2024, Iringa

Post a Comment

0 Comments